Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, April 3, 2012

KAULI YA WEMA SEPETU KUHUSU DIAMOND KUKATAA KUPOKEA HELA ZAKE DIAMONDS ARE FOREVER


Wema Sepetu.

.

B12 na Wema , mwenye nguo ya njano ni Dj Fetty.
Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu leo amepata nafasi ya kuzungumza Exclusive na XXL ya CLOUDS FM na kuzungumza kuhusu mambo kadhaa ikiwemo ishu ya juzi kwenye show ya DIAMONDS ARE FOREVER  Mlimani City Dar es salaam.
 
Kwa kuanza Wema Sepetu amekanusha stori kwamba alikwenda nyumbani kwa kina Diamond ili amchukue waondoke pamoja kwenda Mlimani City, inadaiwa Diamond aliikataa hicho kitu kwa sababu hakutaka kujihusisha na Wema kwa vyovyote vile kwa kuwa wao sio wapenzi tena na hawajawa na ukaribu kwa kipindi kirefu.
 
Sentensi nyingine ya Wema kukanusha hizo stori ni pamoja na kukiri kwamba hapafahamu nyumbani anapoishi Diamond kwa sasa, nyumba aliyokua anaifaham ni sehemu waliyokua wanaishi wote tu.
 
Muda mfupi baada ya Wema kuyatoa hayo maneno, Diamond alipiga simu Live na kuthibitisha kwamba ni kweli Wema alimfata nyumbani kwao siku ya show ili waende wote, hakupenda na alijiepusha kutofanya chochote ili show yake isiharibike siku hiyo, alipotoka nje akaambiwa Wema ameshaondoka.
 
Kuhusu ishu ya Diamond kukataa kupokea pesa ya Wema, Wema amesema “ule ni ushamba, alichofanya ni uswahili, mimi nitazidi kuwa shabiki wa Diamond, nitazidi kuwa shabiki wake na kumsupport lakini abadili tabia yake, alichofanya ni uswahili… sisi sio maadui kuna leo na kesho, nilipompelekea ile hela ni kwa sababu Naupenda sana wimbo wa mawazo sana aliokua anauperform kwa wakati huo, ndio maana alipoupiga niliamka na kwenda kumpa pesa”
 
Alipoulizwa kama bado ana hisia za kimapenzi kwa Diamond, Wema amesema kwa sasa hana hisia zozote kwa Diamond na hayuko tayari hata kuanza ukurasa mpya wa kimapenzi na yeye.
 
kwa kumalizia Wema amekanusha kauli ya Diamond aliyoitoa kwamba Wema anajitafutia umaarufu kupitia jina lake, kwa kusema “mimi natafuta jina kupitia jina lake, c’moooooon mimi nimekua staa since 2006 Diamond ameanza kujulikana 2007, plsss Diamond umenidisappoint…..jirekebishe”

Hii ndio Tattoo ya Wema.

.
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA MILLAD AYO UKIIPENDA ACHA UJUMBE