Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, April 6, 2012

special thankx for support our model

Dear All,
 Thank you very much for your support from day one.  You were the reason of the amazing turnup  of 486 participants on the 25th March.  Tonight its Tanzanians day during the South African fashion week showcase and we are still count up on your support and we ask for your best wishes for our models (Anastazia Gura, Victoria Casmir, Victor Casmir, & Bernard Chizi who will join international models on the runway) and our Tanzanian designers (Doreen Noni - Eskadobird, Evelyn Rugemalira, Jamila Vera Sway and Julie Lawrence - Fahari) who will showcase their garments).
Kind regards,
Lucy T. Ngongoseke
Managing Director,
Tabasamu Pr Consultancy
Mobile: +255 754 602674

MWANAMITINDO Anastazia Gura aliyechaguliwa na mbunifu mkubwa wa mavazi wa Afrika Kusini Olive Clandle kuonesha mavazi yake ameeleza kufurahishwa na hatua hiyo.
  Anastazia akihojiwa na waandishi wa habari wa hapa Afrika Kusini alisema kuwa akiwa kama mwanamitindo chipukizi kuchaguliwa kuonesha mavazi ya mbunifu huyo ni hatua kubwa kwake.
  Alisema kuwa kwa kitendo cha kuchaguliwa bila hata ya kuonekana katika jukwaa ni dhahiri kuwa anavya vigezo vya kutosha na hivyo amepania kufika mbali zaidi.
  Anastazia alichaguliwa mara tu baada ya kuonekana akijaribisha nguo za wabunifu wa kitanzania wanaoshiriki katika onesho hilo la wiki ya mavazi.
  Alifika nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuonesha mavazi ya wabunifu watatu wa kitanzania waliochaguliwa na mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese.
 

Lakini hata hivyo alijikuta akichaguliwa kuonesha na mavazi ya mbunifu Olive Clande huku akiwa ndio kwanza anaingia katika tasnia ya uanamitindo huku  akiwa hajawahi hata kutembea jukwaani.
  Hatua hiyo imeonekana kuwashangaza waandishi wa habari wa mitindo na hata wanamitindo wengine waliopo hapa Afrika Kusini kwa kuwa mara zote mbunifu huyu hupendelea kuwatumia wanamitindo wenye majina makubwa.
  Akizungumzia hatua hiyo Millen alisema kuwa Anastazia na vigezo vyote vinavyotakiwa kuwa mwanamitindo na ndio maana ameweza kupatiwa nafasi hiyo kirahisi.

  “Ni kwamba ili uweze kuchaguliwa inatakiwa angalau uwe na vigezo vya kimataifa ili kumwezesha mbunifu kuchagua mtu wa kumuoneshea nguo zake” alisema Millen.
Mwisho