Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, April 4, 2012

Uuuuh i cant wait !!!! lolz .Halima Mdee atangaza kuolewa na Joshua Nassari = kutoka Gazeti la Habari Leo

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.“Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo,” alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru juzi katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa chama chake katika uchaguzi huo.

Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

“Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi,” alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia.

Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa.

Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni.

“Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili,” alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu’.

Chadema ina idadi kubwa ya wabunge vijana ambao hawajaoa, ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’; wa Ubungo, John Mnyika; wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na sasa Nassari.