Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, April 13, 2012

Mapinduzi Guinea Bissau

 
Siku chache tu baada ya wanajeshi wa Mali kurudisha mamlaka kwa utawala wa kiraia, mapinduzi mengine ya kijeshi yametokea katika nchi ya Guinea Bissau.

Wanajeshi nchini humo wamevamia makaazi ya Waziri Mkuu usiku wa kuamkia Ijumaa ya tarehe 13 Aprili na kuwakamata wanasiasa kadhaa. Hadi sasa Waziri Mkuu huyo, Carlos Gomes Junior aliyekuwa anajianda kwa duru ya pili ya uchaguzi hajulikani alipo.

Mapinduzi hayo yametokea ikiwa zimebaki wiki mbili tu kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais ambao kampeni zake zilikuwa zianze leo na kumalizika tarehe 26 mwezi huu.

No comments:

Post a Comment