Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, April 16, 2012

HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA KATIKA KILI MUSIC AWARDS 2012


 Msanii wa muziki wa Hip Hop, Profesa Jay wa Mitulinga ukipenda umuite Joseph Haule akiwa na meneja wa Wanaume TMK Saidi Fela wakiwa tayari kumkabidhi Roma tuzo yake ya msanii bora wa Hip Hop.
 Msanii wa muziki wa Hip Hop, Profesa Jay wa Mitulinga ukipenda umuite Joseph Haule akiwa na meneja wa Wanaume TMK Saidi Fela wakimkabidhi Roma tuzo yake ya msanii bora wa Hip Hop.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hip Hop Roma akiwashukuru Wanzania mara baada ya kupata tuzo yake ya msanii bora wa Hip Hop. Pembeni ni Msanii mwenzake Izo Busines akifurahia mwenzake kupata tuzo. Ambapo aliipeleka tuzo hiyo kwa mama yake mzazi aliyeko kwao mjini Tanga.
 Muigizaji wa Kundi la Komedy, Mjuni a.k.a Mpoki ambaye alikuwa ni mshereshaji wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania. Akiwa amevaa vazi lenye asili ya Mtanzania lililobuniwa mbunifu Manju Msika ambaye ofisi zake zipo maeneo ya Keko jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Taarab Khadija Kopa akiwasha moto stejini.
 Msanii wa Taarab Khadija Kopa akiwasha moto huku akisindikizwa na watoto wake.
 Meneja wa Kinywaji cha Konyagi na mwakilishi wa Redds wakikabidhi Ommy Dimpoz pamoja na Ali Kiba tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana.
 Ommy Dimpoz na Ali Kiba wakifurahia tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana.
 Mwakilishi wa msanii Jaguar kutoka nchini Kenya akiwa na tuzo ya msanii huyo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki uitwao Kigeu geu.
 Shemejiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, hii ndiyo salamu ambao msanii wa kundi la Orijino Komedy Wakuvanga alikuwa akiwasalimu wageni.
 Msanii wa Taarab Khadija Kopa akiwa na mumewe pamoja na bintize wakati akishukuru mara baada ya kupata tuzo.
 Wasanii wa Wanaume TMK wakiwajibika huku Chege na Temba wakikamua.
Wasanii wa kundi la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba, wakiwajibika na Bibi Cheka.
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (katikati) akiwa na wageni wengine.
 Wageni wakifuatilia kwa makini utoaji huo wa tuzo.
 Waandishi wa Habari wakifuatilia.
 Wabunifu wa mavazi Ali Remputula akiwa na mama wa mitindo Asia Idarous.
 Tumependeza.
 Suka akiwa na wife wake Zuena.
 Wageni kutoka Airtel nao hawakuwa nyuma.
 Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam inapofanyaka Kilimanjaro Music Award 2012 leo tarehe 14/4/2012 kuanzia saa 2 usiku panavyoonekana. 
 Kwa ndani, viti vilivyopangwa.
Steji inavyong'aa.
 PICHA HABARI NA MATUKIO KWA HISANI YA CARTHBERT WA HABARI MATUKIO.

No comments:

Post a Comment