matukio ya mwisho ya mazishi ya Marehemu Steven Kanumba kupitia sitelite zake zilizokuwa zikimalizia kazi hiyo kwenye makaburi ya Kinondoni baada ya kutoka pale Leaders,kama inavyoonyesha kwenye picha hii ya kwanza.
Waombolezaji wa msiba wa Marehemu Steven Charles Kanumba wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu kwenye kaburi, tayari kwa kumpumuzisha katika nyumba ya milele kwenye makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo jioni , Kanumba atakumbukwa kwa kazi yake nzuri katika tasnia ya filamu hapa nchini, ambapo alijitangaza na kuitangaza nchi vyema ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kupitia filamu zake nyingi alizoigiza.
(MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN)
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa akiuaga mwili wa mwanaye kwa mara ya mwisho kabla ya kuzikwa rasmi katika makaburi ya Kinondoni.
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa na ndugu wa karibu wakiaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho makaburini Kinondoni.
Waombolezaji wakitayarisha jeneza la marehemu Steven Kanumba tayari kwa kuliweka kaburini.
Mmoja wa waombolezaji akibebwa baada ya kupoteza fahamu makaburini.
Wajenzi wa kaburi la marehemu wakichanganya Sementi kwa ajili ya kufukia.
Maqma wa Marehemu Steven Kanumba akiweka shada la maua mkaburini
Wafanyakazi wa msalaba mwekundu wamefanya kazi ya ziada kutoa huduma ya kwanza kwa waombolezaji
Maskari wa kusimamia usalama wakiweka uzio kwa ajili ya kuhakikiosha usalama katika mazishi hayo.
Polisi wakiweka ulizi wa kutosha katika mazishi hayo.
Kamanda wa Kanda Maalum ya kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waombolezaji makaburini Kinondoni.
Umati huu wote uko makaburini na wengine kama unavyoona wamepanda kwenye miti ili mradi tu waone mazishi ya mpendwa wao Steven Kanumba.
Mwanamitindo maarufu mtanzania anayefanya kazi zake za mitindo nchini Marekani Millen Magese akienda kuweka shada la Maua kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba.
PICHA HABARI NA MATUKIO KW AHISANI YA FULL SHANGWE.
PICHA HABARI NA MATUKIO KW AHISANI YA FULL SHANGWE.
No comments:
Post a Comment