Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, April 5, 2012

BREAKING NEWS: LEMA AVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA LEO ASUBUHI.

 

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini mheshimiwa Godbless Lema wa CHADEMA avuliwa ubunge na mahakama asubuhi hii ya leo jijini Arusha, hali ya utulivu na amani imeripotiwa kutawala Mjini huko na kilichokubaliwa ni kwamba wamesema kuwa hawakati rufaa wanasubiria uchaguzi mwingine.

      NIKUKUMBUSHE TU NI KWAMBA

Kesi hiyo iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Agness Mollel, Mussa Mkanga na Happy Kivuyo ambao walikuwa wanamtuhumu mbunge huyo kwamba alitoa kauli za udhalilishaji, matusi na kashfa kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dk Batilda Burian imetolewa hukumu na jaji Gabriel Rwakibarila.