Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, April 9, 2012

TAMASHA LA PASAKA REBEKA MALOPE AFANYA KWELI


Mwimbaji wa muziki wa injili Rebecca Malope kutoka nchini Africa Kusini akiimba huku akisindikizwa na gwiji wa nyimbo za injili Rose Muhando  wa pili kutoka kushoto mara baada ya kufanya onyesho la kukata na shoka kwenye tamasha la muziki la Pasaka jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, wanamuziki wengi wa kimataifa wametumbuiza katika tamasha hilo wakiwemo Solomon Mukubwa mkutoka Congo DRC, Joshua Sekereti kutoka Zambia, Emi Kosgei kutoka Kenya na  Anastazia Mukabwa kutoka Kenya, hapa nyumbani walikuwepo Rose Muhando mwenyewe, Christine Shusho na wengine

 Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchini Afrika Kusini Rebecca Malope akiimba katika tamasha la pasaka linalofanyika kwenye uwanja wa taifa usiku huu, tamasha hilo limeanza tangu mchana na waimbaji wengi wameshaimba na kutoa burudani ya kutosha kwenye uwanja wa Taifa
 Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchini Afrika Kusini Rebecca Malope akicheza huku Msanii wa muziki Dokii akicheza naye katika tamasha la muziki la Pasaka kwenye uwanja wa Taifa.
 Mwimbaji Rose Muhando akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wa Taifa usiku huu.
 Rose Muhando akiimba na kucheza na kundi lake jukwaani.
Rose Muhando akiimbisha mashabiki kwenye uwanja wa taifa ambao wameonekana kuchanganyikiwa sana na nyimbo zake hasa wimbo wa "Utamu wa Yesu"


WAZIRI BERNALD MEMBE AZINDUA ALBAM YA SOLOMON MUKUBWA "UTUKUFU KWA MUNGU" UWANJA WA TAIFA

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akiangalia albam ya Mwanamuzikiwa muziki wa injili Solomon Mukubwa inayokwenda kwa jina la (Utukufu wa Mungu)mara baada ya kuizindua rasmi jioni hii kwenye Tamasha la Pasaka linalofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Alex Msana mwandaaji wa tamasha hilo, Solomon Mukubwa mwimbaji wa albam hiyo na Askofu Gamanywa.


Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe wa tatu kutoka kulia akielekea jukwaani kwa ajili ya kuzindua albam hiyo, kutoka kushoto ni Richard Kasesela, Askofu Gamanywa na kulia ni John Melele

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akiongozwa na Mkurugenzi wa Msama Promotion kuelekea jukwaani kwa ajili ya kuzindua albam ya Solomon Mukubwa.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe wa pili kutoka kulia akiongoza na na Alex Msama Mwandaaji wa Tamasha la Pasaka, kutoka ushoto ni Richard Kasesela Mwenyekiti wa kamati ya ushauri Madini na Askofu Gamanywa.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akisalimiana na mwanamuziki Emi Kosgei kutoka Kenya, kulia ni Alex Msama.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akisalimiana na waimbaji wa muziki wa injili kutoka kulia ni Christine Shusho, Upendo Nkone na Upendo Kirahiro
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili kabla ya kuzindua albam hiyo.
 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akizindua albam hiyo, kutoka kulia ni  Alex Msama, Solomon Mukubwa, na John Melele wakishuhudia tukio hilo.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akitoa ahadi yake ya kuinunua shilingi milini 10 ambapo pia 
Mh Bernald Membe akicheza na mke wake Dorkas Membe mara baada ya kuzindua albam hiyo
Mashabiki lukuki wakiwa katika uwanja wa taifa jioni ya leo
Mwimbaji Solomon Mukubwa akiimba jukwaani kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa albam yake utukufu kwa mungu.

TAMASHA LA PASAKA LAPAMBA MOTO UWANJA WA TAIFA JIONI HII

Mwimbaji wa muziki wa injili Solomon Mukubwa akiingia katika uwanja wa Taifa mchana huu tayari kwa kukonga nyoyo za mashabiki wa nyimbo za ijili katika tamasha kubwa la Pasaka jiji ni Dar es salaam
Mwimbaji Upendo Kirahiro akifanya vitu vyake jukwaani
Mwanamuziki Rebecca Malope kutoka nchini Afrika Kusini akielekeza jambo katika tamasha hilo kabla ya kupanda jukwaani leo hii kwenye uwanja wa Taifa.
Waimbaji wa muziki wa injili wakiingia uwanjani kutoka kulia ni Christina Shusho, Upendo Kirahiro na Upendo Nkone.
Wanamuziki Rose Muhando akiingia uwanjani huku akiwa ameongozana na waimbaji kutoka nchini Kenya Tutuma kushoto na Emi Kosgei..
Elistone Angai naye yumo katika tamasha hilo leo hii.
Kundi lingine likitumbuiza katika tamasha hilo.
Mashabiki lukuki wakiwa uwanjani

Mashabiki wakiimba  na kucheza kwa nguvu katika uwanja wa Taifa
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA JOHN BUKUKU WA FULL SHANGWE.

No comments:

Post a Comment