Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, April 3, 2012

Wenge el Paris live!


Unamkumbuka Marie Paul “Le Roi Soleil”???? Huyu hapa anaendeleza libeneke na Wenge El Paris yake….kwa wanaoijua vizuri historia ya wenge musica jina Marie Paul halitakuwa geni kwao,huyu ni mmoja kati ya waanzilishi wa wenge musica original kabla hata Jb Mpiana hajajiunga na wenge,walikuwa yeye werrason,didier masela….na wengine,Jb alikuja baadae japo ujio wake ndio ulioitoa wenge mafichoni na kuipatia utambulisho rasmi congo nzima na africa kwa ujumla kufuatia nyimbo zake mbili Mulolo na Kin e bouge ambao uliipatia wenge tuzo ya kwanza ya muziki ndani ya congo na kuwapatia changamoto kubwa zaiko langalanga ambao kabla yaujio huu wa wenge na nyimbo hizo walionekana kama hawana mpinzani ndani ya Kinshasa,wenge ikaja kivingine na kufuta utawala huo wa zaiko wa muda mrefu kwenye muziki wa congo.
Marie Paul na wenzake kina Aime Buanga ndio walikua watu wa mwanzo kujiondoa wenge na kuasisi hii wenge el paris ambapo baadae kina Aime Buanga wakajitoa tena ndani ya wenge el paris na kumuachia jahazi Marie Paul ambae anaendeleza libeneke kama nilivyosema hapo juu kama kawa japo amekua hasikiki sana na wenge yake kama wenge mbili maarufu,ya mpiana na werrason ambazo ndio zinafanya vizuri na ziko juu,lakini El Paris hawavumi tu ila wamo!