Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, April 23, 2012

HII NI MARA YA PILI KWA ELIZABETH MICHAEL ( LULU) KUPANDISHWA KIZIMBANI



Mahakama ya hakimu mkazi KISUTU jijini Dar es Salaam leo imeahirisha kesi ya tuhuma za mauaji inayomkabili ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’ dhidi ya aliyekuwa mwana filamu mahiri Marehemu STEVEN KANUMBA.

Wakili wa Upande wa Serikali ELIZABETH KAGANDA akizungumza mahakamani hapo amedai Upepelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba kesi hiyo itatajwa tena mei 7 mwaka huu.

Umati mkubwa ulijitokeza katika mahakama hiyo kwa lengo la kufuatilia mwenendo mzima wa kesi hiyo ambayo imevuta hisia za watu wengi hapa nchini.

Hii ni mara ya Pili kwa ELIZABETH MICHAEL kupandishwa Kizimbani kosa la mauaji ya mwana filamu huyo mnamo April 7 mwaka huu eneo la Sinza Vatican Jijini Dar es Salaam.
ASANTE CARTHBERT ANGELO KWA PICHA HIZI

3 comments:

  1. sasa mlimleta wa nini kama upelelezi bado !!!!
    na ana haki ya kupata zamana kama bado yuko ndani

    ReplyDelete
  2. Dhamana haitolewi kwa baadhi ya makosa na mojawapo ni kosa la tuhuma za mauaji.

    ReplyDelete
  3. Dhamana haitolewi kwa baadhi ya makosa ya kisheria na mojawapo ni kosa la mauaji

    ReplyDelete