Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, April 24, 2012

BAADA YA KUZUSHIWA KAFARIKI DUNIA, HIKI NDICHO ALICHOKIONGEA MWIGIZAJI SAJUKI.


Sajuki kabla ya kuumwa.
Baada ya stori kuenea kwamba Mwigizaji Juma Kilowoko maarufu kama SAJUKI amefariki dunia, amejitokeza mwenyewe na kuziamplfy hizo stori.

Sajuki amesema “mimi ni Sajuki ninaezungumza, unajua nikwambie siri moja, nilikaa nilifikiria, kwanza nilishituka sana mwenyewe japokua naona kama wananiongezea uhai, wanaiombea dua ya uhai”
Katika sentensi nyingine Sajuki amesema “unajua majuzi kati mke wangu Wastara alikua anawaambia watu juu ya kuumwa kwangu na namna gani tunavyohitaji watu watusaidie sasa pengine maadui wakaona kwamba watanzania wameshituka sana wameona watatusaidia, wenyewe ndio wakaamua kuchafua chafua vitu kama hivyo kwa hiyo ni habari za kizushi, mimi niko fesh tu hapa sasa hivi”
Amesema “niko kwenye mpango wa kufanya movie yangu mpya ambayo nitaingia location nitaisimamia, hata hizo habari zilipoanza kutoka nilikua kwenye maandalizi ya movie yangu.

Nikashtuka nikasema heee nimekufa niko location jamani hata watu niliokua nao wakawa wanashangaa, wakati ukifika utafika mwenyenzi Mungu akiamua kunichukua atanichukua, sawa mimi naumwa lakini sio kwenye hiyo hali ambayo watu wanaielezea, pamoja na kuumwa kwangu sasa hivi nipo kama Rambo napigana bado”


HABARI HII NI KWA HISANI YA MILLAD AYO.

No comments:

Post a Comment